MAHASIMU WA SIASA(ODINGA NA KENYATA) NCHINI KENYA WAKUTANA KWA MAZUNGUMZO


KENYA: Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa NASA Raila Odinga wanakutana na kufanya mazungumzo katika jengo la ‘Harambee House’ huko Nairobi.

Lengo la mazungumzo hayo bado halijajulikana lakini viongozi wawili hao wanatarajiwa kufanya mkutano na vyombo vya habari muda wowote kuanzia sasa

Ikulu ya Kenya ilitangaza kuwa Rais Kenyatta ataongea na vyombo vya habari majira ya saa 5 asubuhi

Awali, Kumekuwa na wito wa majadiliano kutoka Marekani na nchi nyingine baada ya Raila Odinga kukataa kukubali Uhuru Kenyatta kama rais wa halali.


No comments