KESI YA KIKATIBA: Amri aliyopewa Mwanasheria Mkuu na Mahakama Kuu ya Tanzania


Leo March 9, 2018 stori ya kimahakama nayokusogezea ni kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania ambapo imemuamuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kuwasilisha majibu yake kuhusu kesi za Kikatiba zilizofunguliwa na wananchi 28 ikiwemo kupinga Jeshi la Polisi kuzuia maandamano.

Akizungumza na waandishi wa habari, Wakili wa wananchi hao Jebrah Kambole amesema mashauri hayo ya Kikatiba ni namba 4 na 6 ya 2018 ambapo yamepangwa kusikilizwa April 5,2018.

Kambole amesema mahakama hiyo ilipanga kuanza kusikiliza mashauri hayo leo March 9, lakini imeshindikana kwa sababu baadhi ya majaji wamepangiwa kesi nyingine.

Kambole amesema kuwa mahakama imemuamuru AG kuwasilisha majibu yake kuhusu mashauri hayo March 21,2018.

“Mashauri haya ya yanapinga sheria mbalimbali ikiwemo kupinga sheria ya uchaguzi, pia Wakurugenzi wa Halmashauri kuwa wasimamia wa Uchaguzi wakati inapaswa kuwepo tume huru ya Uchaguzi,”.

Wakili Kambole amesema kwenye shauri namba 4 wananchi hao 28 wanapinga sheria za Jeshi la Jeshi la Polisi na vyama vya siasa ambazo zinatoa muongozo wa kuzuia mikutano ya Kisiasa na kusababisha madhara mengi kwa wananchi.

“Hivyo kimsingi tunapinga sheria hizo ambazo ni kandamizi na zinakiuka misingi ya Katiba, ibara ya 18 Uhuru wa kujieleza kufanya mamuzi juu ya maisha ya Watanzania na nchi,”.

Pia sheria hizo zinakiuka haki ya kusikilizwa kwa watu wanaotoa taarifa kwa Jeshi la Polisi wakitaka kuandamana wanapata amri kabla ya kusikilizwa, hivyo kimsingi tunaangalia uhalali wa hizo sheria kwa Katiba yetu ya Tanzania.

“Kwa mujibu wa Ibara ya 16 inatoa majibu kwa mtu yoyote anayeona sheria imekiukwa ana wajibu wa kuleta shauri Mahakamani.

Mahakama imeyapanga mashauri
hayo kuyasikiliza April 5 2018

Sourse : Millard  ayo

No comments