KUTOKWA NA DAMU NYINGI WAKATI WA HEDHI (MENORRHAGIA)

KUTOKWA NA DAMU NYINGI WAKATI WA HEDHI (MENORRHAGIA). Hili ni taitizo ambalo huwakumba wanawake wengi katika nyakati tofautitofauti.
Mwanamke hutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi pia inaweza kudumu kwa wiki moja na zaidi.
Hali hii isipopatiwa ufumbuzi huweza kuleta madhara makubwa sana kwa mwanamke ambayo hupelekea vifo.
Katika hali fulani sababu ya kutokwa na damu nyingi inaweza isijulikane.
Zipo sababu kuu zinazosababisha hali hii.
SABABU ZA MSINGI
Zifuatazo ni sababu kuu ambazo huchangia tatizo hilo.
1.Kutokuwepo kwa usawa wa vichocheo (Hormonal imbalance)
Vichocheo vya oestrogen na progesterone hutakiwa kuwa katika usawa ili viweze kufanya kazi yake ipasavyo, Matumizi ya vichocheo katika kupanga uzazi(vijiti/contraceptive pills) huweza kubadili Hali ya vichocheo na kusababisha hali hiyo kutokea
Kama hali hii itatokea ukuta wa mfuko wa mimba hutoa damu nyingi isiyokawaida.
2. Matatizo ya ovari.
Ovari ni sehemu muhimu sana katika katika kuandaa na kukuza yai na badae kutolewa likiwa kamili kuingia katika mirija ya fallopia tayari kwa safari kuelekea mfuko wa kizazi.
Kama ovari zitashindwa kutoa mayai basi tatizo huwa ni upingufu wa kichocheo kiitwacho progesterone hicho yai haliwezi kutoka kwenye ovari na hali hii husababisha damu nyingi kutoka wakati wa hedhi.
3. Uvimbe kwenye shemu ya kizazi (Fibroids)
Fibroids siyo saratani bali huwa ni uvimbe wa kawaida ambao hubaki sehemu moja (benign), ambayo hutokea katika umri wa uzazi.
Na hii husababishwa na vichocheo kutokuwa katika usawa na huweza kusababisha damu nyingi kutoka wakati wa hedhi.
4. Vimbe ndogondogo kwenye kizazi.
Huwa ni vimbe ndogo sana katika mfuko wa uzazi.
Hutokea kwa wanawake katika umri wa kuzaa kutokana na  vichocheo kuongezeka.
5. Magonjwa ya kurithi.
Matatizo ya damu kutoganda kutokana na hii husababishwa na ukosefu wa vigandishi vya damu.
6. Matatizo ya kiafya.
Maambukizi katika njia ya kizazi kama Pelvic Inflammatory Diseases(PIDs)
Je nani yuko hatarini kukumbwa na hali hii?
Makundi yafuatayo yako katika hatari ya kukumbwa na tatizo hili.
1. Wale waliovunja ungo hasa mwaka mmoja wa kwanza
2.Wanawake wanaokaribia ukomo wa hedhi kati ya miaka 40-50 wako hatarini katika mabadiliko ya vichocheo.
ZIJUE DALILI NA VIASHIRIA VYA TATIZO HILI (Menorrhagia)
1.Kutumia pads moja ama zaidi kila  saa kwa mfululizo wa masaa kadhaa.
2. Uhitaji wa kuamka usiku kubadili pad.
3.Damu kutoka nyingi zaidi ya  siku nne  wakati wa hedhi.
4.Kutoa mabonge ya damu wakati wa  hedhi zaidi ya siku moja.
5.Kutoshiriki shughuli za kila siku kutokana na damu nyingi kutoka
6.Dalili za kuishiwa damu, kama kuchoka, ama kupumua kwa shida.
MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA ENDAPO HATUA MADHUBUTI HAZITACHUKULIWA.
1.Upungufu wa iron ambayo ni madini muhimu katika damu ambapo husaidia katika kubeba hewa ya  oksijeni, kukosekana ama kupungua  kwake maisha  huwa  hatarini.
2. Maumivu makali wakati wa hedhi ambayo wakati mwingine  huhitaji  kutumia dawa za kutuliza maumivu.

No comments