USAJILI WA LINE ZA SIMU KWA KUTUMIA ALAMA ZA VIDOLE:

Mfumo wa majaribio ya kusajili line za simu kwa kutumia alama za vidole vya watumiaji umezinduliwa rasmi hii leo, Alhamisi jijini Dar es Salaam ambapo Mpango huo utahusisha mikoa ya Iringa, Tanga, Singida, Pwani, Dar es salaam na Zanzibar.

Mfumo huo unaanza kwa majaribio kabla ya kuwa endelevu kwa nchi nzima lengo likiwa ni kuweka udhibiti katika mitandao na udanganyifu katika usajili wa namba za simu kwa watu kutumia vitambulisho visivyo sahihi ama cha mtu mwingine.

No comments