KIDATO CHA NNE WALIO CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI WATAKIWA KUFANYA YAFUATAYO

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2018 wataanza muhula
wa kwanza tarehe 16 Julai, 2018. Wanafunzi wote wanapaswa kuripoti katika Shule
aliyopangiwa kwa muda uliopangwa. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi
ya siku 14 kuanzia tarehe ya mwisho ya kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na
mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.
Mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, anapaswa kupakua (Download)
fomu ya kujiunga na shule husika kwenye mtandao. Mwanafunzi hapaswi kwenda
kuchukua fomu ya kujiunga katika shule aliyopangwa na haruhusiwi kupiga simu. Aidha,
wanafunzi waliopangwa kwenye Vyuo vya Elimu ya Kati inabidi kufanya UTHIBITISHO
kuanzia tarehe 17 Juni, 2018 hadi ifikapo tarehe 8 Agosti, 2018 wa kukubali kujiunga na
Kozi na Vyuo walivyopangiwa kwa njia ya mtandao. Uthibitisho huo utafanyika kupitia
tovuti ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ya www.nacte.go.tz katika
kiunganishi kinachoitwa Uthibitisho TAMISEMI. Mwanafunzi atakayeshindwa
kuthibitisha kozi na chuo alichopangiwa, nafasi yake itachukuliwa na wanafunzi wengine.
Mwanafunzi atakayetaka kufanya mabadiliko ya kozi na chuo alichopangiwa ataruhusiwa
kufanya hivyo kuanzia tarehe 9 Agosti, 2018 hadi 23 Agosti, 2018 kupitia tovuti ya NACTE
ya www.nacte.go.tz.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, Vyuo vya Ufundi na
Vyuo vya Kati vinavyosimamiwa na NACTE kwa mwaka 2018 pamoja na fomu za
kujiunga na shule (joining instructions) inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais -
TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi

No comments