WEKA DEGREE PEMBENI
Na Edward Aloyce Geremiah
call 0754501179
       0752561499

Habari watanzania na vijana wa kitanzania mlioko vyuoni na mlioko mtaani .awali ya yote na penda kumshukulu mwenyezi Mungu kwa zawadi ya uhai

MADA
Weka degree pembeni ni hoja iliyo kizungumkuti kwa watanzania wengi (hasa vijana wasomi/walioko vyuoni )
wengi tumeambukizwa dhana ya kuajiliwa zaidi ya kujiajili,dhana ya kuifikili kesho zaidi ya leo ambayo hujaitendea haki,dhana ya kulalamika pale tunapo kosa ajila kila eneo kwa sabab zozote zile .ukweli huu hapa.

MFUMO
Vijana wengi wasomi wameandaliwa na mfumo DUME( yaani mfumo wa kuamini kwamba bila elimu ya ngazi flani huwezi miliki mali na fedha,huwezi kubalika katika jamii)
mfumo tunao uzungumzia hapa ni mfumo mzima wa elimu haumwandai kijana wa kjitanzania kujitegemea/na kama una mwandaa kujitegemea basi ni dhahili kuwa kijana ajajua lengo la mfumo .
kwanini mfumo?
leo tanzania kijana aliye tumia miaka 13 yaani ( elim ya msingi miaka 7,sekondari 4 na A-level 2) mbali na nadhalia hakuna ambacho kijana anaweza kukifanya kwa ajili ya kumuingizia kipato ambacho kitatokana na elimu yake (yaani hawezi hata kushika tanakirishi (computer na kandika jina lake) kutokana na elimu yake ukiachilia mbali maswala ya afya ya kimwi.

Kijana huyu akikosa nafasi ya kwenda chuo kikuu anaumia sana na kuona kapoteza safari yake ya miaka 13 bure
hata hivyo jiulize, je kwa mtoto ambaye yuko gereji ya ufundi magari je ndani ya muda huo wote si amekwisha bobea kwenye maswala ya ufundi?
leo hata muhitimu wa degree ya kwanza mashilika yanayo toa kazi haya mamini kwenye vigezo vya maombi utasikia UZOEFU WA MIAKA MITANO KAZINI ,(Na wakijitahidi kumpa ajila watampa miezi 6-7 ya induction course) swali hapa je ile elimu ya miaka 16 yote iko wapi je si bola sanaa zaidi ya ile ya miezi 6-7? binafsi nakosa majib

JE PESA ZIKOWAPI?

Wasomi watanzania pesa ziko kwenye mifumo isiyo rasmi mifumo hiyo ni ipi na iko wapi ?
mifmo hiyo iko kwenye jamii zetu na mifumo yenyewe ni fursa mbalimbali zinazojitokeza kila siku kwenye jamii zetu.
hili lina jionyesha wazi kuwa hata matajili wakubwa duniani wanaijia pesa  kuanzia mtumiaji wa chini (mfano bakhresa ana uza mandazi hadi ya Tsh 200@) hii yote ni kuisaka pesa


Kipi Kifanyike

1. mfumo badili aina ya utoaji elimu

2.Mama elimu anaye tupatia vyeti ni muhimu kwa maana ya tunu ya kile tulicho kifanya miaka kadhaa ndani ya mfumo na kukifahuru vizuri
Wasomi wa tanzania tuweke vyeti kando tujihusishe na shughuri ndogo ndogo kwenye jamii ndizo zinazo gusa maisha ya kila siku ya watanzania ........
Tusijikweze kwenye jamii kwa kupuuza kazi flani ambayo yawezekana ungeifanya kwa muda wako wa ziada unge kuwa haupo hapo ulipo..
Mkemia MEDIA
Youth for better vision organization



<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<ITAENDELEA>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

No comments