Onyo la obama kwa matumizi mabovu ya mtandao

Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama ameonya kuhusu matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii wakati wa mahojiano yasiyo ya kawaida tangu aondoke madarakani mwezi Januari. 

Alionya kuwa vitendo kama hivyo vinachanganya uelewa wa watu katika masuala magumu na kusambaza uvumi. 

Obama alihojiwa na Prince Harry katika BBC Radio 4. 

Obama alisema wale walio katika nyadhifa za uongozi wanastahili kuwa waangalifu wakati wanaandika katika mitandao. 

Alielezea wasi wasi kuhusu siku za usoni ambapo ukweli utapotoshwa na watu watakuwa wakisema, watakuwa wakisoma na kusikiliza vitu ambavyo vitakuwa vikiridhisha maoni yao. 

Sasha Obama alikuwa wapi wakati ya hotuba ya mwisho ya babake? 
Bw. Trump amelaumiwa kwa kutumia mtandao wa Twitter kupindukia licha ya yeye kusisitiza kuwa inamruhusu kuwasiliana moja kwa moja na watu wa Marekani.

No comments