UJUMBE WA GAVANA WA BENKI KUU(BOT) Profesa Benno Ndulu
aloyce blog
"Huyu ndiye mrithi wangu"
Nimaneno ya gavana wa banki kuu ya Tanzania (BOT) Prof. Benno Ndulu alipokuwa akimtambulisha gavana mteule Profesa Florens Luoga Jana jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa mpango wa pili wa taifa wa huduma jumuishi za fedha kwa mwaka 2018/2022
Alisema pamoja na hayo tathimini iliyofanyika inaonyesha kuwa kiwango cha wanachi waliokaribu na huduma za fedha wameongezeka hadi kufikia 86% ya watanzania (watu wazima) mwaka 2017 ikilinganishwa na 29% ya mwaka 2012
Profesa Ndulu ambaye ni mwenyekiti wa baraza LA taiga LA huduma jumuishi za kifedha anayemaliza muda wake amesema idadi ya watanzania wanaotumia huduma za kifedha kupitia asasi za kifedha na mitandao ya simu wameongezeka kutoka 17% ya mwaka 2009 had 65% ya mwaka 2017.
Kwa upande wake, aliyekuwa mgeni rasmi kassimu majaliwa alimshukuru profesa ndulu kwa kazi nzuri na kubwa aliyoifanya. Alisema "uwepo wa uchumi imara na unaokuwa kwa kasi ni miongozi mwa sababu zinazo sababisha ukuaji wa haraka wa sekta ya fedha...."
Chanzo : mtanzania fikra yakinifu
Post a Comment