UTATA JUU YA KIFO CHA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA

Jeshi la polisi mkoani Iringa linawashikilia watuhumiwa wawili kufuatia kifo cha kutatanisha cha mwanafunzi wa kike wa kidato cha sita Sundi George aliyekuwa akisoma katika shule ya sekondari Mwembetogwa.

Mwanafunzi huyo alikutwa amefariki katika miti ya kugema pombe ya ulanzi huku mwili wake ukiwa na kamba shingoni.

Akitoa taarifa za awali kwa vyombo vya habari  kamanda wa polisi mkoani hapa ACP Juma Makanya amesema mnamo March 12 mwaka huu akiwa na sare za shule alitoka nyumbani kwao kuelekea shuleni lakini hakurudi hadi mwili wake ulipopatikana  maeneo hayo.

Aidha kamanda bwire amesema wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo huku akiwaomba wananchi kutoa taarifa kwa mtu yoyote wanayehi amehusika katika tukio hilo.

No comments