VIONGOZI TSNP WASEMA TAARIFA ZA ,POLISI (IRINGA NA DAR ES SALAAM )HAZIENDANI WAHITAJI KUMSIKILIZA NONDO KWANZA

Mtandao wa wanafunzi nchini Tanzania (TSNP) umesema taarifa za nini hasa kilichomsibu  Nondo zinakinzana.

"Sisi bado hatuamini Uchunguzi uliofanywa na polisi kwa kuwa hatujamsikia Nondo akiongea na kile tulichoelezwa na polisi mkoani Iringa na hiki tulichokisikia leo kwa polisi Dar es Salaam haviendani", Msemaji wa TSNP Helllen Sisya aliiambia BBC.

Taarifa za kupotea kwa Nondo katika mazingira ya kutatanisha ziliibuka tarehe 6 Machi baada ya Nondo kutuma ujumbe kwa mmoja wa marafiki zake usiku wa manane akisema kuwa usalama wake uko hatarini.

Hali hiyo ilipeleka taharuki miongoni mwa wanafunzi wenzake na jamii kwa jumla huku wengi wakidhani kuwa Nondo alikuwa ametekwa.

No comments