ZITTO APINGANA NA MAJIBU YA SERIKALI ..AIBUA MAPYA YA MWAKA 2013 WIZARA YA UJENZI

  Na Aloyce.
Zitto kabwe amefungukaa haya kupitiaa ukurasa wake  wa facebook....

Watanzania wenzangu,

Kwenye ripoti yake, CAG hajasema popote kuwa TZS 1.5trn zimeibiwa. Alichosema leo Ikulu ndio msimamo wake uliopo kwenye Taarifa yake ukurasa wa 34. Fedha hizo HAZIONEKANI kwenye matumizi ya Serikali ya mwaka 2016/17.

Ndio maana tunahoji zipo wapi. Tunataka Ukaguzi Maalumu ili kuhakiki majibu ya Serikali na kujua hela zetu zipo wapi. Hilo tu, hakuna lingine.

Vitisho vya hatua za kisheria ni tambo tu za watawala, hazina maana yeyote. Kumsimamisha CAG Ikulu na kumhoji mbele ya Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ni kumtisha CAG, ni kinyume na misingi ya Katiba yetu. Ripoti ya CAG ikishakuwa mbele ya Bunge sio Ripoti ya Executive tena. Ni mali ya Bunge. Kama Rais ana majibu aende akayaseme Bungeni mbele ya PAC.

Rais sio wa kumchekea chekea anapovunja misingi ya nchi yetu. Ni lazima ADHIBITIWE na Taasisi za Kikatiba ikiwemo Bunge. Rais leo amekosea. CAG naye amekosea kwenda Ikulu.

Watanzania sikilizeni, mimi nimekuwa Mwenyekiti wa PAC/POAC miaka 8, ninajua kusoma, kuchambua na kutafsiri Taarifa ya CAG. TZS 1.5trn hazina maelezo, hazipo Benki Kuu na Maelezo ya Naibu Waziri Fedha leo ni kujikosha tu.

Nikiwa Mwenyekiti wa PAC, Mwaka 2013 Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli alikutwa na Hoja ya ukaguzi ya TZS 252 bilioni ya ujenzi wa barabara hewa ambayo mpaka sasa haijajibiwa na utaikuta kwenye Hoja za CAG za mwaka 2016/17. Hivyo ni Kawaida yake kutoheshimu sheria za Fedha na kutojibu Hoja za Ukaguzi.

Kama Serikali ina uhakika kabisa hii hoja ya TZS 1.5trn haipo inipeleke mahakamani hata leo. Nitawashinda hata Jaji akiwa mmoja wa majaji wapya walioapishwa leo.

Mimi siogopi. Nitasema UKWELI daima fitina kwangu mwiko.

Zipo wapi TZS 1.5trn?

1 comment:

  1. Sikuwahi kuamini kitu kama hiki kingeweza kunitokea hadi ndoa yangu ilipokaribia kuisha kabisa.

    Mume wangu alibadilika ghafla. Mwanaume ambaye hapo awali alinipenda na kunijali akawa baridi, asiyejali, na mwenye hasira bila sababu. Aliacha kuonyesha nia katika ndoa yetu, akaniepuka kabisa, na hatimaye akaniomba talaka. Nilivunjika moyo kwa sababu nilimpenda mume wangu kwa moyo wangu wote.
    Mambo yalizidi kuwa mabaya aliponizuia kila mahali — WhatsApp, Facebook, Instagram — kana kwamba sijawahi kuwepo. Nililia kila usiku nikijiuliza nilifanya nini kibaya.
    Siku moja, rafiki wa karibu alinitembelea na kunitambulisha kwa mtu wa kiroho anayeitwa Dkt. Dawn. Kwa kweli, mwanzoni nilikuwa na shaka, lakini niliamua kumweleza kila kitu kwa sababu sikuwa na chochote cha kupoteza.

    Dkt. Dawn alinisomea mambo ya kiroho, na nilishtuka. Alifichua siri kuhusu ndoa yangu na maisha yangu binafsi ambayo hakuna mtu aliyejua. Kila kitu alichosema kilikuwa sahihi 100%. Kisha akafichua kwamba mwanamke mwingine alikuwa amemloga mume wangu. Mwanamke huyu alikuwa akimtembelea mara nyingi, na kwa upumbavu niliamini ilikuwa kuhusu kazi tu.
    Dkt. Dawn alinisaidia kuvunja uchawi na akafanya ibada yenye nguvu ya kurejesha upendo kwa ndoa yangu.
    Kwa mshangao wangu mkubwa, muda mfupi tu baadaye, mume wangu alinifungulia kizuizi mwenyewe na kuanza kunipigia simu na kunitumia ujumbe mwingi, akiniomba nimsamehe na nirudi nyumbani. Mwanzoni nilimpuuza kwa sababu ya maumivu aliyonisababishia, lakini hatimaye alirudi nyumbani akiwa na zawadi na machozi machoni mwake akiomba nafasi nyingine.
    Leo, ndoa yetu ni imara zaidi, yenye furaha zaidi, na yenye amani zaidi kuliko hapo awali. Mapenzi kati yetu yanahisi upya kabisa.
    Kana kwamba hiyo haitoshi, Dkt. Dawn baadaye alinisaidia na ibada ya ujauzito kwa sababu tulikuwa tumejitahidi kwa miaka mingi kupata watoto. Ndani ya wiki 8, nilipata mimba kiasili, na leo tumebarikiwa na wavulana wawili wazuri wenye afya njema.
    Nitaendelea kushukuru milele.
    Ukihitaji: Uchawi wa mapenzi wa kuungana tena na mpenzi wako wa zamani
    . Usaidizi wa kurejesha ndoa
    . Tamaduni za ujauzito za kupata mimba
    . Usaidizi wa kiroho kwa kesi za mahakamani au kupona urithi
    . Mwongozo na ulinzi wa kiroho
    Ninapendekeza sana Dkt. Dawn. Ushuhuda wangu ni wa kweli, na furaha yangu leo ni uthibitisho. WhatsApp yake: +2349046229159. dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete