BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU YA TOA UTALATIBU KAMILI WA NAMNA YA KUOMBA MKOPO/VIGEZO NA MASHARTI

BOFYA HAPA KU APPLY


BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU 
 
MWONGOZO WA UTOAJI MIKOPO NA RUZUKU KWA WANAFUNZI KWA MWAKA WA MASOMO 2018/2019
1.0 MAELEKEZO MUHIMU KWA WANAFUNZI WOTE WAOMBAJI MIKOPO
Waombaji mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2018/2019, wanakumbushwa yafuatayo:
(i) Dirisha la uombaji mikopo kwa njia ya mtandao kwa mwaka wa masomo 2018/2019 litafunguliwa kuanzia Alhamisi, Mei 10, 2018 hadi Jumapili, Julai 15, 2018.
(ii) Kusoma na kufuata taratibu za maombi katika Mwongozo huu wa mwaka wa masomo 2018/2019.
(iii) Kuhakikisha maelezo unayoyatoa katika fomu ya maombi ya mkopo, yawe sawa na maombi ya udahili wa chuo. Unasisitizwa namba ya Mtihani wa Kidato cha Nne iwe sawa na iliyopo kwenye maombi ya mkopo na udahili wa chuo.
(iv) Kuhakikisha nyaraka zote za maombi ya mkopo unazowasilisha zimehakikiwa na mamlaka husika.
(v) Kuhakikisha vyeti vyote vya kuzaliwa/vifo na vingine vinathibitishwa na Mamlaka ya Vizazi na Vifo (RITA) au ofisa aliyechaguliwa, ili kuthibitisha uhalali huo. Hata hivyo, Ofisa Wilaya Ustawi wa Jamii (DSWO) anaweza kuidhinisha ripoti ya kifo cha mzazi kutoka kwa mamlaka ya kijiji au kata.
(vi) Kuhakikisha taarifa kuhusu wazazi/walezi na mdhamini (kazi, anuani ya mwajiri namba ya simu, anuani ya posta) ziko kamili na sahihi. Waombaji mikopo ambao wazazi wao ni viongozi waliotajwa katika Kanuni ya Uongozi wa Umma, hawapaswi kuomba kwa sheria ya mwaka 1995.
(vii) Waombaji ambao wazazi/walezi ni wamiliki wa biashara, mameneja wakubwa katika mamlaka zinazotambulika zenje usajili, hawaruhusiwi kuomba mkopo.
(viii) Waombaji wakamilishe fomu zao kwa usahihi na mara wanapowasilisha hawataweza kurekebisha taarifa hizo iwapo huwakujaza kwa ufasaha.
(ix) Waombaji wanatakiwa kutunza nakala za maombi ya mkopo waliyowasilisha Bodi ya Mikopo kwa matumizi mengine (kama itahitajika).
(x) Waombaji wanakumbushwa kuzingatia muda wa kutuma maombi.
2.0 KWA UFUPI
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilianzishwa chini ya kifungu cha sheria namba 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi Julai, 2005. Bodi ya Mikopo pamoja na majukumu mengine, ina jukumu la kutoa mikopo au ruzuku kwa wanafunzi wenye sifa na wahitaji. Dirisha la uombaji
2
mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 litafunguliwa Mei 10, 2018 na kufungwa Julai 15, 2018.
3.0 USTAHIKI
Sheria na Kanuni za Bodi ya Mikopo hutoa sifa na vigezo kwa ujumla kwa wanafunzi wahitaji wa mkopo. Mwombaji stahiki na mhitaji, anaweza kuomba mkopo/ruzuku ili kugharamia sehemu ya gharama au gharama zote za masomo ya elimu ya juu.
3.1 Uhitaji
Mbali na sifa za jumla, vigezo vya ziada vinasema mwanafunzi mhitaji asizidi umri wa miaka 33 katika kipindi anachoomba mkopo, ambaye ni:
(i) Yatima (ambaye amepoteza wazazi wote wawili) au aliyepoteza mzazi mmoja. Awasilishe cheti cha kifo kilichothibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA).
(ii) Mwombaji mwenye ulemavu uliothibitishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO), au Wilaya (DMO), au chombo chochote kilichoidhinishwa kuthibitisha uhalali wa hali hiyo.
(iii) Mzazi mwenye ulemavu uliothibitishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO), au Wilaya (DMO), au chombo chochote kilichoidhinishwa kuthibitisha uhalali wa hali hiyo.
(iv) Mwombaji anayetoka katika familia ya kipato cha chini au kaya masikini, ambaye elimu ya sekondari au diploma alifadhiliwa na taasisi inayotambulika. Waombaji wa aina hii wanatakiwa kutoa ushahidi kutoka taasisi huaika kuthibitisha udhamini huo.
3.2 Sifa za jumla zinazotambulika kisheria
Vigezo vya jumla kwa mwombaji mkopo, anatakiwa awe:-
(i) Mtanzania.
(ii) Lazima awe ameomba mkopo kupitia mfumo wa maombi ya mkopo (OLAMS).
(iii) Lazima awe amedahiliwa kutoka taasisi ya elimu ya juu, kwa muda wote. Isipokuwa wanafunzi waliodahiliwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Open University of Tanzania OUT).
(iv) Asiye na ufadhili mwingine.
(v) Mwanafunzi anayeendelea na chuo, mwenye matokeo/ripoti za matokeo yanayoonyesha ufaulu wa masomo yake, ili kumwezesha kuendelea mwaka ujao au kwenda hatua nyingine ya masomo.
(vi) Kwa mwanafunzi mnufaika ambaye anataka kuomba tena mkopo baada ya kusitisha masomo/chuo, anatakiwa alipe asilimia 25 ya fedha alizotumia kabla hajaomba mkopo mpya (malipo ya 25% ya mkopo wa awali si dhamana ya kupangiwa mkopo).
3
3.3 Vigezo na stahiki nyingine
(i) Mkopo utatolewa kwa kuangalia uhitaji na programu
(ii) Waombaji wapya lazima wawe wamehitimu elimu ya Kidato cha Sita (ACSEE) au Stashahada ndani ya miaka mitatu, kuanzia mwaka 2016 hadi 2018. Wanafunzi wanaoendelea hawahusiki na kigezo hiki.
(iii) Kusipokuwa na kuongeza kwa kipengele chochote mwaka husika, kiasi anachopangiwa mwanafunzi kitakuwa kile kile kwa miaka yake ya masomo.
4.0 MAKUNDI YA PROGRAMU Baada ya kuainisha waombaji wahitaji, na kuonyesha taratibu katika kipengele 3.1 na 3.2 hapo juu, makundi ya programu zifuatazo yenye vipaumbele yatapewa mikopo kulingana na uwapo wa fedha.
4.1 Kundi la Kwanza
Kozi katika kundi la kwanza ni:-
(i) Ualimu wa Sayansi (Fizikia, Kemia, Baiolojia na Tehama) na Ualimu wa Hisabati na Masomo ya Biashara.
(ii) Sayansi za Afya (Udaktari, Upasuaji Meno, Madawa ya Mifugo, Ufamasia, Uuguzi, Ukunga, Shahada ya Sayansi katika Prosthetikia na Mifupa, Shahada ya Sayansi katika Mazoezi ya Viungo, Shahada ya Sayansi ya Afya na Maabara, Shahada ya Sayansi ya Maabara na Matibabu na Shahada ya Sayansi ya Teknolojia ya Mionzi).
(iii) Sayansi za Kilimo na Misitu
(iv) Programu za Uhandisi (Ujenzi, Mitambo, Umeme, Uchimbaji, Madini na Utayarishaji, Utengenezaji Nguo, Kemikali na Usindikaji, Kilimo, Chakula na Usindikaji, Uundaji Magari, Viwanda, Umeme na Mawasiliano, Vipimo na mizani , Usafirishaji Majini, Teknolojia ya Uhandisi wa Baharini, Programu za Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mitandao, Mazingira na Mipango Miji, Usindikaji na Huduma Baada ya Mavuno.
(iv) Sayansi ya wanyama na uzalishaji
4.2 Kundi la Pili
Kozi katika kundi hili ni:
(i) Programu za Msingi za Sayansi (Shahada ya Sayansi kwa ujumla, Shahada ya Sayansi na/katika Wanyama, Mimea, Kemia, Fizikia, Baiolojia, Baiolojia ya Viumbe Vidogo, Baiolojia ya Mifugo na Bioteknolojia, Uvuvi na Mifugo, Sayansi ya Mazingira na Uhifadhi, Jiolojia, Jiologia ya Petroli, Mafuta ya Kemikali, Matibabu, Hisabati na Takwimu, Sayansi ya Mazingira na Usimamizi, Afya na Mazingira, Baioteknolojia na Maabara, Wanyamapori na Uhifadhi, na Kompyuta).
(ii) Programu ya Sayansi ya Ardhi (Usanifu, Mazingira na Usanifu, Ubunifu wa Ndani, Uchunguzi wa Jengo, Uchumi wa Ujenzi, Mipango Miji na Mikoa, Usimamizi wa Ardhi na Vigezo, na Teknolojia ya Geospatial).
4
4.3 Kundi la Tatu
Kozi katika kundi hili ni pamoja na Sanaa, Binadamu, Sheria, Lugha. Kozi nyingine zote ambazo hazijaorodheshwa katika makundi mengine, zitaangukia katika kundi hili. Shahada nyingine zote ambazo hazikutajwa kwenye Kundi la Kwanza, la Pili au la Tatu, zitajumuishwa katika kundi hili.
5.0 VIPENGELE VYA UTOAJI MKOPO, KIPIMA UWEZO NA FEDHA INAYOPANGIWA
Bodi ya mikopo inaweza kulipia gharama za vipengele vyote hapo chini au baadhi;
(i) Gharama za Chakula na Malazi
(ii) Ada
(iii) Vitabu na Viandikwa
(iv) Mahitaji Maalumu ya Kitivo
(v) Utafiti
(vi) Mafunzo kwa Vitendo
5.1 Kipima/King’amua Uwezo
Kipima uwezo kitatumika kuonyesha umuhimu wa uhitaji wa kifedha wa mwombaji. Malipo ya ada iliyolipwa shule za sekondari (CSEE, ACSEE) na diploma, ni kigezo kimojawapo kinachoangaliwa kuwa na uwezo wa kuchangia gharama za elimu ya juu, vingine ni uyatima, ulemavu, udhamini na familia masikini.
Kwa maana hiyo, uhitaji utapimwa katika tofauti kati ya gharama za jumla za mwaka za programu ya elimu katika chuo husika na gharama iliyotumika kugharamia elimu ya sekondari au diploma za elimu ya juu na uwezo wa mwombaji alioubainisha.
5.2 Mgawanyiko wa vipengele vinavyokopeshwa
Upangaji mikopo kwa mwombaji aliyefanikiwa kupata mkopo utagawanywa kwa kuanzia na gharama za chakula, malazi, ada, vitabu na viandikwa, mahitaji ya vitivo, utafiti, na mwisho mafunzo kwa vitendo kulingana na kiasi kilichobakia kutoka vipengele vilivyotangulia.
5.3 Kiwango cha Ada
Kiwango cha juu cha ada kwa waombaji wote watakaofanikiwa kupata mikopo kitakuwa sawa na gharama za ada zinazolipwa katika vyuo vikuu vya umma.
5.4 Mwanafunzi anayeendelea na masomo, ambaye ni mnufaika wa mkopo
Kwa wanafunzi wote wanufaika wanaoendelea na masomo, wataendelea kupokea mikopo kama awali kulingana na ufaulu wa mitihani yao. Wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao ni wanufaika wa mikopo HAWARUHUSIWI KUOMBA MKOPO isipokuwa kwa wale wanafunzi wahitaji ambao awali hawakupangiwa mikopo.
5.5 Chakula na Malazi, Vitabu na Viandikwa, Ada, Gharama za Mafunzo kwa vitendo na Mahitaji Maalumu ya Vitivo
Malipo ya chakula na malazi, vitabu na viandikwa, mafunzo kwa vitendo na gharama za utafiti, yatalipwa moja kwa moja kwa mwanafunzi wakati ada na mahitaji maalumu ya vitivo yatalipwa moja kwa moja kwenye taasisi ya elimu ya juu.
5
6.0 TARATIBU NYINGINE KATIKA UTOAJI MIKOPO
6.1 Wajibu wa Wadhamini, Wazazi na Kamishna wa Viapo
Wazazi/Wadhamini wahakikishe usahihi wa taarifa zao ambazo zimewasilishwa katika fomu ya maombi ya mkopo kabla ya kusainiwa. Wadhamini wanatakiwa kuhakikisha mikopo inarejeshwa na lazima waelewe mahali wakopaji walipo, walipe mikopo yao yote na ikitokea hawajamaliza kulipa, mdhamini atalazimika kulipa mkopo huo.
6.2 Urejeshaji Mikopo
(i) Baada ya kumaliza au kusitisha masomo ya elimu ya juu, mnufaika wa mkopo atatakiwa kurejesha mkopo kwa makato si chini ya asilimia kumi na tano (15%) ya mshahara wake wa kila mwezi.
6.2.1 Mahitaji ya Urejeshaji Mikopo
6.2.1.1 Tozo ya kulinda thamani ya fedha
Ili kuhakikisha Mfuko wa Ukopeshaji unakuwa endelevu, tozo ya kulinda thamani ya fedha itakatwa asilimia sita (6%) kwa mwaka, tangu tarehe mnufaika aliyoanza kupokea mkopo.
6.2.1.2 Ada ya usajili
Bodi ya Mikopo itakata asilimia moja (1%) ya ada ya usajili kwa mwanafunzi mnufaika.
6.2.1.3 Ada ya makato ya adhabu
Ikiwa mnufaika atashindwa kulipa mkopo baada ya kipindi cha neema cha miezi 24 baada ya kuhitimu masomo yake, ataongezewa makato ya adhabu ya asilimia kumi (10%).
7.0 Kuhama Chuo au Programu Ndani ya Chuo
HESLB haitafanya malipo ya mkopo kwa wanafunzi ambao watahama vyuo kwa hiari yao wenyewe. Baada ya kupokea uthibitisho wa uhamisho wa chuo kutoka kwa mamlaka husika, uhamisho wa mkopo utafanyika. Hakuna uhamisho wa mkopo utakaofanyika zaidi ya siku tisini (90) baada ya usajili. Uhamisho wa mkopo utafanyika kulingana na kiasi cha mkopo kilichopangwa awali kwa mwanafunzi husika.
Orodha ya waombaji waliopangiwa kwenye taasisi za elimu ya juu
HESLB itazingatia maombi ya mkopo kutoka kwa wanafunzi waliopangiwa katika taasisi za elimu ya juu na kuwasilishwa Bodi na mamlaka husika.
8.0 Jinsi ya kuomba mkopo
6
Maombi yote ya mkopo yatafanyika kupitia Mfumo wa Maombi ya Mikopo (OLAMS). Waombaji wote wa mikopo WANAKUMBUSHWA kutumia namba ya Kidato cha Nne sawa na itakayotumika wakati wa kuomba kujiunga na chuo.
Baada ya kukamilika kwa mchakato wa maombi ya mkopo mtandaoni, waombaji watapaswa kutoa nakala za fomu za mombi na mikataba ya mkopo kwenye mtandao, kugonga mihuri sehemu husika, kusaini fomu, kuweka nyaraka zinazohitajika na kuziambatanisha kwenye mtandao wa OLAMS kabla ya kutuma maombi hayo kwa njia ya EMS kwa:
Mkurugenzi Mtendaji, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
S.L.P 76068, 14113 DAR ES SALAAM, TANZANIA
Waombaji wanakumbushwa kutunza nakala ya fomu ya maombi, viambatanisho vilivyowasilishwa na risiti ya EMS iliyotumiwa kutuma maombi yao kwa kufuatilia HESLB endapo italazimika.
9.0 Ada ya Maombi ya Mkopo
Waombaji wanapaswa kulipia ada ya maombi ya mkopo kiasi cha shilingi elfu thelathini (30,000/=) kupitia Benki ya NMB na CRDB.
Kwa maelezo zaidi tembelea: https:/olas.heslb.go.tz
9.1 Mwisho wa Kupokea Maombi
Dirisha la Maombi ya Mkopo kwa mwaka 2018/2019 litafunguliwa kuanzia Mei 9, 2018 hadi Julai 15, 2018.
Orodha ya Waombaji Watakaopangiwa Mikopo
Orodha ya waombaji watakaofanikiwa kupangiwa mikopo itawekwa kwenye tovuti: www.heslb.go.tz
10.0 KUKATA RUFAA
Waombaji ambao hawataridhika na kiwango cha mkopo walichopangiwa, wanaweza kukata rufaa kwa kukamilisha fomu za rufaa kwenye mtandao. Maelezo zaidi yatatolewa baadaye.
11.0 MAULIZO NA MALALAMIKO
Waombaji au wanufaika wa mikopo wenye maswali au malalamiko, watapaswa kufuata taratibu zilizotolewa kwenye dirisha la maombi ya mkopo.
12.0 WANAFUNZI WA SHAHADA YA UZAMILI NA UZAMIVU
7
Wanafunzi watakaokopeshwa kwa mwaka wa masomo 2018/2019, waliodahiliwa kusoma shahada za uzamili na uzamivu, lazima wawe na sifa za jumla zilizowekwa katika kipengele cha 3.2 hapo juu.
12.1 Wanafunzi wa Uzamili na Uzamivu (Wahadhiri)
Mbali na sifa za jumla, waombaji wa shahada ya uzamili na uzamivu, lazima wawe na vigezo maalumu ambavyo ni:
(i) Wanapaswa wawe na Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu na kiwango cha chini cha ufaulu kiwe ni Daraja la Pili la Juu (Kwa waombaji wa Shahada ya Uzamili) au Shahada ya Uzamili na kiwango cha chini cha ufaulu kiwe Daraja la Pili la Juu (Kwa waombaji wa Shahada ya Uzamivu).
(ii) Wanapaswa kuwa wahadhiri wa taasisi za elimu ya juu watakaodahiliwa kusoma masomo yao katika taasisi za elimu ya juu zinazotambulika nchini Tanzania.
(iii) Wanapaswa kuteuliwa na kupatiwa kibali kutoka kwa mwajiri ambaye ni Mkuu wa Chuo wa taasisi husika.
(iv) Wanapaswa kuwa wameanza kurejesha mikopo yao ya awali angalau kwa muda usiopungua miezi kumi na miwili (12) au kurejesha kwa mkupuo mkopo stahiki kwa waombaji ambao awali walinufaika na mikopo ya wanafunzi.
(v) Mwajiri lazima awe amesaini mkataba kati ya HESLB na taasisi husika ya elimu ya juu.
12.2 Wanafunzi wa Shahada ya Uzamili na Uzamivu Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST)
Ili kuimarisha uwezo wa taifa katika utafiti, TEHAMA na uvumbuzi, HESLB inatoa mikopo kwa wanafunzi wanaodahiliwa kusoma Shahada za Uzamili na Uzamivu katika masomo yanayohusu Sayansi katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST).
Wanafunzi watakaokopeshwa kwa mwaka wa masomo 2018/2019, wanapaswa kuwa na sifa za jumla zilizowekwa katika kipengele 3.2 hapo juu.
Mbali na sifa za jumla zilizowekwa katika kipengele 3.2 hapo juu, waombaji wa Uzamili na Uzamivu NM-AIST, lazima watimize vigezo vingine maalumu:
(i) Wawe wamedahiliwa katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) katika Shahada ya Uzamili au Shahada ya Uzamivu katika mojawapo ya kozi za kipaumbele hapo chini:
 Sayansi za Maisha.
 Uhandisi wa Sayansi ya Hisabati na Kompyuta.
 Uhandisi wa Sayansi ya Habari na Mawasiliano.
8
 Sayansi ya Malighafi, Nishati, Maji na Mazingira.
(ii) Lazima awe ni mwajiriwa katika taasisi ya umma na amefanya kazi kwa muda usiopungua miaka miwili (2).
(iii) Lazima awe amedhaminiwa na mwajiri wake kuhusu urejeshaji wa mkopo
(iv) Lazima awe ameanza kurejesha mkopo wa awali angalau kwa muda usiopungua miezi kumi na mbili (12) kwa mkupuo kwa jumla ya miezi kumi na mbili (12) kama hapo awali alikuwa mnufaika wa mkopo kutoka Bodi ya Mikopo.
(v) Marejesho ya mikopo ya wanafunzi wa Shahada za Uzamili na Uzamivu wa NM-AIST, yataanza mara tu baada ya kumaliza mwaka wa kwanza wa masomo, kwa mwajiri kuwasilisha Bodi ya Mikopo makato ya kila mwezi kutoka kwenye mshahara wa mnufaika.
12.3 Wanafunzi wa Shahada ya Uzamili waliodahiliwa katika Shule Kuu ya Sheria ya Tanzania (LASCOT)
Wanafunzi wa Shule Kuu ya Sheria wanaostahili kukopeshwa kwa mwaka wa masomo 2018/2019 lazima wawe wametimiza masharti yafuatayo:
Lazima wawe na sifa za jumla zilizowekwa kipengele cha 3.2 hapo juu.
Mbali na sifa za jumla zilizowekwa kipengele cha 3.2 hapo juu, waombaji wa mikopo katika Shule Kuu ya Sheria Tanzania (LASCOT) lazima wawe na vigezo maalumu, ambavyo ni:
(i) Awe amehitimu Shahada ya Sheria si zaidi ya miaka mitatu nyuma (2015 hadi 2017).
(ii) Mikopo itatolewa kwa waombaji wahitaji tu kulingana na matokeo ya kipima uwezo wa mwombaji.
(iii) Ikiwa mwombaji ni mnufaika wa mkopo awali, ambaye mkopo wake umekwishaiva, anapaswa kuwa amerejesha kiasi chote kilichoiva kinachostahili kurejeshwa.
Kulingana na uwepo wa fedha, mikopo ya Shule Kuu ya Sheria inaweza kutolewa kwa kiasi kidogo au chote katika maeneo yafuatayo:
(i) Vitabu na gharama za viandikwa.
(ii) Ada ya mafunzo
9
12.4 Vipaumbele kwa Wanafunzi wa Stashahada na Kozi zisizo za Shahada
Miongozo na sifa za kustahili kupata mikopo kwa wanafunzi wa Stashahada na Kozi zisizo za Shahada chini ya programu iliyochaguliwa (iliyothibitishwa) itatolewa baadaye.
12.5 Viwango vinavyotumika kwa Wanafunzi wa Uzamili na Uzamivu
12.4.1 Chakula na Malazi
Bodi inatoa mikopo kwa ajili ya chakula na malazi kwa kiasi cha shilingi elfu kumi (10,000/=) kwa siku wakati wa mafunzo chuoni au wakati wa kukusanya data.
12.4.2 Gharama ya Vitabu na Viandikwa
Kiasi cha shilingi laki tano (500,000/=) kwa mwaka kwa vitabu na viandikwa hutolewa kwa wanafunzi wa Shahada ya Uzamivu. Kiasi cha shilingi 200,000 kwa mwaka kwa ajili ya vitabu hutolewa kwa wanafunzi waliodahiliwa katika Shule ya Sheria ya Tanzania.
12.4.3 Ada ya Mafunzo
HESLB inatoa mikopo ya ada ya mafunzo kwa asilimia mia moja (100%) kulingana na kiwango cha ada cha Taasisi ya Elimu ya Juu husika isipokuwa kwa Shule ya Sheria Tanzania (LASCOT).
12.4.5 Gharama za Utafiti
HESLB inatoa asilimia mia moja (100%) ya gharama za utafiti kulingana na viwango vinavyotumika na Taasisi ya Elimu ya Juu husika, ambavyo huweza kuidhinishwa mara kwa mara. Viwango vinavyotumika ni kiasi cha shilingi milioni mbili (2,000,000/=) kwa mwaka kwa Shahada ya Uzamili na shilingi milioni tano (5,000,000/=) kwa mwaka kwa Shahada ya Uzamivu.
SEHEMU B: UTOAJI WA RUZUKU
13. RUZUKU
13.1 Vipengele vya Ruzuku
Kulingana na uwepo wa fedha, ruzuku inaweza kutolewa katika maeneo yafuatayo:
(i) Ada ya mafunzo
(ii) Gharama za vitabu na viandikwa
(iii) Gharama za mahitaji maalum ya kitivo
(iv) Gharama za mafunzo kwa vitendo
10
(v) Gharama za utafiti
13.2 Vigezo Stahiki
Utoaji wa ruzuku utazingatia vigezo vifuatavyo:
13.2.1 Awe amedahiliwa katika Taasisi ya Elimu ya Juu inayotambulika Tanzania na athibitishwe ni mlemavu kwa barua kutoka kwa Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) au Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO) au chombo chochote kilichoidhinishwa kuthibitisha ulemavu huo.
13.2.2 Awe amejaza fomu za maombi ya ruzuku na aziwasilishe katika ofisi husika kwenye taasisi ya elimu ya juu aliyopo.
13.2.3 Ruzuku kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo itatolewa kutokana na kufaulu katika mitihani, inayomwezesha mwombaji kuendelea na masomo kwa mwaka unaofuatia. (Ruzuku haitatolewa kwa wanafunzi wanaohama kutoka chuo kimoja kwenda kingine au kwa wale wanaorudia mitihani).
Wanafunzi watakaopatiwa ruzuku kwa mwaka wa masomo 2018/2019, waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu, lazima watimize vigezo vilivyowekwa katika kipengele 3.2 hapo juu.
Tangazo kwa ajili ya Maombi ya Ruzuku litatolewa kwa taasisi za elimu ya juu Oktoba, 2018.
Imetolewa na:
Mkurungezi Mtendaji,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Mei, 2018

No comments